6 mins read

IJUE ZAIDI SHULESOFT

Shulesoft ni nini?

Shulesoft ni mfumo uliotengezwa kwa ajili ya kurahisisha uendeshaji wa shule na kuleta matokeo chanya kwenye shule yako kitaaluma, kukuza mapato na kuboresha mawasiliano kati ya shule na wazazi. Shulesoft ni rahisi kutumia na inatunza taarifa za shule unazoziweka kwenye mfumo bila kupotea. 

Faida za kutumia Shulesoft

Kuongeza makusanyo ya mapato

Hii ni kwa kupitia kufanya malipo moja kwa moja na control namba ambayo mfumo unatengeneza kwa ajili ya wazazi kwa hiyo, ada inapolipwa inaenda moja kwa moja kusoma kwenye mfumo. Hii inapunguza kazi ya kujaza taarifa moja moja kwenye daftari. Pia mfumo unaweza kumzuia mzazi kuona matokeo kama hajalipa ada au hajamaliza kulipa ada, hii itamfanya mzazi alipe kiwango kinachotakiwa ili aone maendeleo ya mwanae. Mfumo una uwezo wa kutuma ujumbe kwa wazazi kuwaandaa na ada ya muhula unaofata, na kama hajamaliza ada ajue anadaiwa kiasi gani.

Kupunguza gharama za operesheni

Faida hii inaonekana kwenye kutengeneza na kutuma taarifa za ada na ripoti za matokeo kwa wazazi kwa kupitia ujumbe wa Whatsapp na kawaida au kwa kutumia Shulesoft Parent Experience App. Hii inapunguza gharama za kuchapa makaratasi, kuprint na kuweka kwenye bahasha kisha kutuma mtoto azifikishe nyumbani ambapo mwanafunzi anaweza asiifikishe. 

Kuongeza mahusiano na wazazi

Mahusiano kati a shule na wazazi ni muhimu kwani mzazi ndio mteja wa shule. Shulesoft inauwezo wa kutumia mzazi ujumbe na taarifa kadhaa zinazomhusu mwanae kama ratiba za mtihani, matukio ya shule, mikutano na kadhalika. Hii inampa mzazi uhakika wa nini anachofanya mwanao akiwa shuleni.

mzazi akitoa shuhuda ya shulesoft.mp4

Kukuza shule kwa kuongeza namba ya wanafunzi wapya

Shulesoft inarahisisha kazi za wafanyakazi wa shule na wazazi pia, hivyo kuongeza muda wa kutangaza shule. Pia wazazi wanaweza kuonyesha wenzao ambao hawajui teknolojia hii na kuwafanya walete watoto wao kwenye shule yako ili kupata hizo faida.

Kupangilia taarifa ili kufanya maamuzi sahihi kama kupima ubora wa wanafunzi na walimu

Taarifa hizi zinapangiliwa na Shulesoft na kutengeneza ripoti maalum kujua ulipo na unapoelekea kama shule. Hivyo kurahisiha kufanya maamuzi kwani taarifa kamili na za uhakika. Mfano kama walimu wanaofanya vizuri waweze kusaidia wanafunzi ambao hawafanyi vizuri na kuongeza bidii kwa walimu wasiofanya vizuri. Taarifa kama hizi unazipata kwenye mfumo hivyo kurahisisha maamuzi wa viongozi wa shule.

Kurahisisha utengenezaji wa ripoti za mtihani.

Pindi mwalimu anapojaza matokeo ya kila mwanafunzi, mfumo unapangilia matokeo kulingana na mpangilio wa necta na kupanga wanafunzi kuanzia wa kwanza mpaka wa mwisho. Hii inapunguza muda wa kufanya kazi hio na mzazi kupata  matokeo ya mwanafunzi mapema zaidi kwa njia ya ujumbe na kuondoa gharama na taarifa za mzazi kutopata matokeo,

Mfumo wa Shulesoft ukoje?

Shulesoft imeundwa na moduli sita zinazohusiana nazo ni; administration(utawala), accounts(uhasibu), academic(taaluma), operation(operesheni), digital learning (mafunzo kidigitali)na communication(mawasiliano). Moduli hizi hushirikiana kwa pamoja na kukuletea suluhisho bora zaidi kwenye shule yako.

1. Utawala (administration)

Hii moduli ni ya kuongeza taarifa za mwanafunzi, mwalimu, na waajiriwa wengine kama dereva,mpishi. Pia kipengele hiki unaweza kuona utendaji wa walimu(KPI) kutokana na ripoti anazoweka kwenye mfumo. Hii inakusaidia kujua walimu bora na wanaohitaji kuongeza bidii na kufanya shule yako iwe bora zaidi. Utawala inakusaidia kuongeza na kupata taarifa zote za mwalimu, mwanafunzi na wafanyakazi wengine za uhakika.

2. Uhasibu (accounts management)

Hii inahusu malipo ya ada,kutengeneza  ankara (invoice), kutengeneza bajeti, kujua na kuweka rekodi ya matumizi ya mapato, kuona mapato ya siku,wiki,mwezi,mwaka na makadirio ya mapato kamili baada ya kupokea ada za wanafunzi wote, malipo na makato ya kiserikali ya mishahara ya wafanyakazi wa shule na kadhalika. Moduli hii huja na kipengele cha ripoti za namna tofauti kama uwakilishaji wa picha wa data au kwa jedwali la maelezo ya jinsi mapato ya shule yalivyotumika na ambacho hakijakusanywa.

3. Taaluma (academic management)

 Kipengele hiki kinahusu kuweka masomo husika kwa kila darasa na walimu waliopangiwa katika kila somo. Pia, kuweka matokeo, kupata ripoti ya matokeo husika kwa kila darasa na kuweza kuweka mpangilio unavyotaka ripoti hizo na atakayezipokea.Taaluma inakupa uwezo wa kutengeneza ripoti kwenye mfumo kwa staili inayotumika na shule yako. Hii inamaanisha, kuweza kuamua nini kionekane au kisionekane kwenye ripoti atakayoipokea mzazi. 

4. Mafunzo kidigitali (digital learning)

 hii inahusu utunzaji wa notsi za wanafunzi, mitihani ya zamani, na darasa mtandaoni pindi mwalimu anahitaji kufundisha wanafunzi walio nyumbani likizo. Moduli hii ilikua ya msaada mkubwa katika kipindi cha korona ambapo shule nyingi zilifungwa kwa muda mrefu na wanafunzi hawakua na namna ya kujifunza na walimu hawakupata namna ya kuwafikia wanafunzi. Mafunzo kidigitali ikawasaidia walimu kuwafikia wanafunzi kwa urahisi, kuwafundisha na kutoa mitihani kidigitali.

5. Operesheni (operations management)

hii inahusu usafiri na mabweni. Kipengele hiki kinategemeana na jinsi shule ilivyo kama ni kutwa au bweni au vyote kwa pamoja. Kwa shule kutwa, usafiri inakuwezesha kusajili basi husika, dereva husika, wanaopanda basi hilo, na ruti zake. Hii inasaidia uongozi wa shule kujua wanafunzi gani na namba ngapi wako kwenye basi gani ili pindi tukio lolote likijitokeza uongozi wapate hizo taarifa kwa haraka kwani makaratasi hupotea. Kwa shule za bweni, hosteli inasajiliwa na msimamizi wake na wanafunzi husika kwenye hosteli hio kwa lengo hilo la kupata taarifa kwa haraka pindi zinapohitajika.

6. Mawasiliano (communications management)

Kipengele hiki kinakutanisha shule na wazazi kwa njia ya ujumbe wa kawaida au ujumbe kwa njia ya WhatsApp. Unaweza kutuma ujumbe wa ada, ujumbe wa tukio, au ujumbe wa ripoti ya mwanafunzi. Mwanafunzi anaposajiliwa na mzazi wake, taarifa za mzazi zinabaki kwenye mfumo na pindi unataka kutuma ujumbe mfumo unakuletea wazazi waliosajiliwa kwahiyo inakuwa rahisi kutuma ujumbe. Mzazi pia anaweza kutuma majibu kuhusiana na ujumbe aliopata na ujumbe huo ukaonekana kwenye mfumo. Moduli hii pia inasaidia kwenye kuwasiliana na wafanyakazi wa shuleni kuhusiana na kikao au taarifa yoyote inayowahusu.

Kwa maswali, maoni, tupigie sasa

+255 748 771 580

JIUNGE LEO…. UKUZE SHULE YAKO!!!

3 thoughts on “IJUE ZAIDI SHULESOFT

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *