8 mins read

RunShule Ni Wezi wa Mfumo wa ShuleSoft, Mahakama Imethibitisha

Taarifa kwa Shule Zote na wadau wote wanaounga mkono ubunifu wa program ya ShuleSoft. Tunapenda kuleta kwa kifupi taarifa kuhusiana na Mfumo wa ShuleSoft na kutoa ufafanuzi kwa mambo mengi ambayo tuliamua kukaa kimya kwa muda kupisha mahakama ifanye kazi yake.

Nini Kilitokea?

Eng. Ephraim Swilla, ni mbunifu wa program mbalimbali katika hii nchi, alianza ubunifu akiwa Chuo Kikuu na kufanikiwa kuaminiwa na serikali kutengeneza mifumo mbalimbali, baadhi ya mifumo hiyo ni

  • Mfumo wa BRELA wa usajili wa majina ya biashara mtandaoni
  • Mfumo wa kukusanya maoni ya katiba mpya ya Tanzania,
  • n.k

Mwaka 2016 alibuni programu ya usimamizi wa shule (School Management Software), na kuipa jina la ShuleSoft, huku akiwa anaendeleza kampuni yake ya INETS aliyofungua akiwa Chuo Kikuu cha DSM, na kuajiri vijana wachache aliomaliza nao Chuo Kikuu, kisha kuwafundisha kazi ili wamsaidie kusimamia kazi zake na pia kusimamia miradi mingine ambayo ndugu Ephraim alibuni. Japo kampuni ya INETS alianza kuisimamia mwaka 2014, tayari alianza akiwa na miradi mingi, ambapo watu aliowaajiri, nao kila mtu alikua na mradi wake aliotengeneza yeye mwenyewe na kuuamini kuwa utaleta mafanikio kwake. Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na

  • karibuSMS – Application ya kutuma SMS
  • File Tracking Software
  • Stock management software
  • Luku meter Remote recharging software
  • Different websites
  • Pension Management System
  • School Management system (ShuleSoft)

Haikushangaza sana, pindi mfumo wa Pension Management System ulipofanya vizuri, Ndugu Erick ambae alikua akiusimamia, aliondoka na kufungua kampuni ya NEXTBYTE , na Ephraim Swilla alibaki kwenye kampuni yake akiendeleza mfumo wake wa ShuleSoft, huku wengine wote wakiwa na project zao walizoziamini.

Changamoto za Kesi zilianzaje?

Siku zilipokwenda, ShuleSoft ilionekana ikifanya vizuri sana kuliko hizo project nyingine zote, jambo ambalo lilifanya wengine wote kuona project zao hazina maana.

Cha kushangaza, badala ya kuunga mkono kazi za ShuleSoft, watu hao wakataka kujimilikisha mfumo wa shulesoft uwe wao, na wakaanza kuongea maneno ya upotovu kwa wafanyakazi wengine, wawekezaji na wabia wa shulesoft, ili kuleta uhasama kati ya Ephraim Swilla na wabia wake, jambo ambalo liliharibu ubora wa ShuleSoft, kuongeza lawama kwa wateja na kupoteza baadhi ya wateja waliokua hawapati huduma vizuri.

Ephraim Swilla alipoona haya, aliamua kuachana kabisa na hawa watu aliowaajiri na wengine kuwafanya hadi wakurugenzi wa kampuni na kuwapa hisa, akaamua kufungua kampuni inayoitwa ShuleSoft Limited ili ahakikishe ubora wa ShuleSoft unarudi, katika viwango anavyotaka, na kuifanya shulesoft ikue Tanzania na Nje ya Tanzania.

Ndipo watu hawa walipoanza kuandika barua za UONGO na UCHONGANISHI, na kuzituma maeneo mbalimbali ikiwemo kwa wateja, wabia, sehemu alizo host mfumo nk , kwa lengo la kuharibu. Haikuishia hapo, wakaandika barua ya madai ya uongo, ikaenda BRELA, kuwarubuni waifungie ShuleSoft, jambo ambalo Ephraim Swilla ilibidi afungue kesi kutaka mahakama iwatie hatiani kwa uovu wanaofanya.

Ilikuaje wakafungua kampuni ?

Wakati wakifanya huu UOVU mkubwa, watu hawa walikua na ajenda moja , kuua na kuharibu ShuleSoft ili wao wafanye biashara, hivyo mwezi wa 12, mwaka 2022, wakafungua kampuni ya RUNSHULE, kwa kuungana na wake zao, na hapo hapo wakaanza kurubuni wateja wa shulesoft.

Watu hao wanao ongoza huu UOVU ni hawa wafuatao

DONATA NICODEMUS RWEGARULILAHuyu ni Mke wa Ndugu YOHANA NASSON, ambae aliajiliwa na ndugu Ephraim Swilla kwenye idara ya IT .
Ndugu YOHANA NASSON ndie kidedea wakuandika barua fake, na kutunga uzushi na uongo wa kuichafua ShuleSoft ili kuharibu jina la ShuleSoft na kudangaya wateja waache shulesoft
Akifanya haya yote kwa nia ovu ili Runshule iwachukue wateja
ELIHURUMA LOMAYANI KIVUYOHuyu ni Mke wa Ndugu AMANI MWAKILASA, ambae aliajiliwa na ndugu Ephraim Swilla kama Accountant wa kampuni ili atunze mahesabu na pia kuwafundisha wateja module account inavyofanya kazi
KELVIN KULWA MBWILOHuyu aliajiliwa na Ephraim Swilla, ili asimamie mfumo na kutengeneza module mpya pamoja na version mpya ya shulesoft , ndipo yeye akajimilikisha kuwa ni yake kwa kukataa kurudisha mfumo kwa ndugu Ephraim Swilla alie mpa kazi
GERALD NOAH MWAKYONDEHuyu nae, alikua mwanasheria ambae Ndugu YOHANA NASSON alikua akimtumia, sasa yeye kwa tamaa mbaya, akaungana KWENDA kumtetea YOHANA kwa kufungua kampuni inayoiba kazi ya Ephraim Swilla `
MWANGATA HAMID MAKAWAHuyu nae ni mwendesha mashtaka pale CMA ambae alipelekewa kesi ili amhukumu ndugu Ephraim Swilla, kuwa awalipe wafanyakazi ambao hakuwaajili, fidia ya zaidi ya Tsh 30,000,000/= , madai ambayo wakili wa Ephraim Swilla aliyatupilia mbali na kesi kufutwa
LAURENT WILFRED SHUKA Huyu nae, aliajiliwa na Ephraim Swilla, ili asimamie mfumo wa ShuleSoft, sasa yeye nae akapewa share kwenye hii kampuni kwani alikua ameshajifunza kuhusu ShuleSoft

Angalia JINSI walivyojigawia share kwenye search hapa chini

Nini kikatokea Mahakamani ?

Mwanzo kabisa wa kesi, mahakama iliwapa watu hawa zuio la muda la kutojihusisha na mfumo wa ShuleSoft au program yoyote ya usimamizi wa shule hadi kesi itapoisha.

Watu hawa kwa ukaidi, walipuuzia amri ya mahakama na kuendelea kufanya kazi, huku wakijificha kutoka kwenye kivuli cha runshule.com na kwenda kwenye kivuli cha forshule.com

Kwa weredi wa Wanasheria wa Ephraim, tulisimamia kesi kuhakikisha kesi inaisha vizuri kabisa , na tarehe 22 Jan, 2024, mahakama ilitoa AMRI ya mwisho kuwa Ephraim Swilla ni mmiliki halali, na watu hawa, wakiwa na kampuni ya INETS, wote waache mara wanachofanya nchini na duniani kote.

Angalia nakala ya amri ya mahakama hapa chini

Je Watu hawa, wanafanyaje wakifika kwa WATEJA ?

Ukifahamu mbinu za WEZI utajua namna ya kujilinda uwe salama. Hizi ni njia wanazozitumia kurubuni watu na wateja ili waungane nao

A) DINI

Watu hawa, hutembea na BIBLIA na pia hutembea na VITABU VYA DINI vya kanisa lao wanakosali. Wakifika kwako , au kwa partner au kwa mteja, kama wewe unapenda dini, basi lazima waongee na wewe kuhusu dini na watakupa vitabu vyao. Kama ni shule ya dini, basi lazima wakusalimu kwa sala za kidini, huku wakiongea kwa upole sana kwa kupangilia maneno.

Kama sio mtu wa kujua watu, ni lazima utawaamini na kuona ni watu sahihi, na tayari wanakua wamekurubuni.

B) KUTIA HURUMA

Wengine husema (Victim Mentality), watu hawa wakija kwako, watajifanya wanatia huruma sana, kwamba wameonewa sana sana, na wanataka uwaonee huruma ili uwasaidie. Mtu yoyote asie jua watu, na ana huruma za karibu, basi ni rahisi kuwasikiliza na kama huwezi kupima ukweli basi ni rahisi kukurubuni.

C) BEI CHEE

Wakishindwa njia hizo mbili, basi wataenda kwenye shule na kuuza mfumo kwa BEI rahisi sana, au watakupa muda wa majaribio bure hata miezi 3 hadi 6 ili wakurubuni.

Shule nyingi zinazopenda vitu POA zimenaswa na huu ujanja wao.

HITIMISHO

ShuleSoft tunatoa rai kwa kila shule inayojihusha na hawa watu, au na mtu yoyote ambae anafanana na hawa, mwenye program ya shule lakini sio yake, ameiba au ame nakili (copy) kwa mtu akajifanya yake, iache mara moja kwani kufanya hivyo ni sawa sawa na kusaidia WIZI (Further infringment) . ShuleSoft haitasita kuchukua hatua stahiki kulinda hakimiliki na kulinda image ya ShuleSoft katika DUNIA.

Zaidi zaidi, tunatoa shukrani za dhati kwa wateja wetu waaminifu, pamoja na wabia wote, wawekezaji na wafanyakazi waaminifu wa ShuleSoft kwa kuwa pamoja nasi kipindi chote cha hawa watu walipokua wakifanya uovu wao.

Sasa, tunaweza endelea kufanya kazi kwa amani, kwani sasa ShuleSoft Limited imesha piga hatua kubwa kama ifuatavyo

  • ShuleSoft imeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wateja kwa shule zaidi ya 470 zikiwa ndani ya mfumo wa shulesoft
  • ShuleSoft imeanza operations katika nchi nyingine za Africa na tayari kuna wateja kutoka nchi nyingine wameanza kujiunga na mfumo wa shulesoft
  • ShuleSoft katika kipindi hicho, imejenga mfumo mpya kabisa, ambao ni bora zaidi na umependwa na shule nyingi sana ukiwa na features mpya nyingi zaidi
  • ShuleSoft imeboresha huduma kwa wateja kwa kiasi kikubwa, kwani sasa tuna kituo cha huduma kwa wateja (CALL CENTER -0748771580) ambacho huudumia wateja kwa weredi mkubwa
  • ShuleSoft imeongeza idadi ya wabia (partners) kama banks , mitandao ya simu na Insurance companies zinazo ongeza wigo mkubwa wa huduma zao ndani ya ShuleSoft
  • Na mengine mengi zaidi. Fika ofisin kwetu, mbezi Beach, ShamoTower, 4th Floor

Kwa hukumu ya ndani zaidi kujua utetezi na yaliyojiri mahakamani, soma hapa chini

https://drive.google.com/file/d/1d0TAjCyuvw6aI_zxxtof5W_xp6oFvxzZ/view?usp=sharing

Kwa habari zaidi, au ukitaka kujifunza kuhusu ShuleSoft au kuwa na maswali zaidi kuhusiana na hawa wezi, wasiliana nami.

Ephraim Swilla

Mkurugenzi wa ShuleSoft.

+255689353642

Asante

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *